Man in the Mirror
"Man in the Mirror" ni jina la kutaja wimbo ulioimbwa na Michael Jackson. Wimbo umetungwa na Siedah Garrett na Glen Ballard na kutayarishwa na Michael mwenyewe akiwa sambamba kabisa na Quincy Jones. Wimbo huu ulipata kushika nafasi ya kwanza nchini Marekani wakati unatolewa mnamo 1988. Wimbo unatoka katika albamu yake ya saba ya mwaka wa 1987, Bad. Maelezo kuhusiana na wimboHuu ni miongoni mwa nyimbo maarufu za Jackson na uliwahi kuchaguliwa kuwa kama Rekodi ya Mwaka katika kipindi cha ugawaji wa tuzo za Grammy Awards. Wimbo huu ulipata kupigwa sana kwenye maredio/matv na kuweza kushika nafasi ya juu kabisa katika chati za Billboard Hot 100 kwa wiki mbili. Kibao hiki kilipata sifa za wastani nchini Uingereza wakati kinatoka, na kiliweza kushika nafasi ya 21 na kuifanya iwe single kutoka katika albamu Bad kutofika kwenye UK Top 20 katika kutolewa kwa mara ya kwanza. Eti baada ya kufa, kunako 5 Julai 2009, kwa kufuatia habari za kifo cha Jackson, wimbo umepata kushika nafasi ya 2 kwenye chati rasmi za UK Singles Chart. Chati
Orodha ya nyimbo
Marejeo
Viungo vya Nje |
Portal di Ensiklopedia Dunia