Programu tumiziProgramu tumizi, maarufu kama Protu (kwa Kiingereza: App), ni programu za tarakilishi zinazotumiwa hasa na simujanja na saajanja na ni tofauti na zile zinazotumiwa na tarakilishi. Mwaka 2009, mwandishi wa makala za teknolojia David Pogue alisema kuwa simujanja mpya zitapewa jina la utani "app phones" ili kuzitofautisha na simu zilizotangulia.[1]. Neno "app", ambalo ni kifupi cha "software application", limekuwa maarufu toka wakati huo. Mwaka 2010 neno hili liliteuliwa na American Dialect Society kuwa "Neno la Mwaka".[2] Programu hizi zina manufaa makubwa kwa watumiaji wa simujanja kwa masuala kama ya muziki, video, michezo kama vile pokeman[3], vitabu, habari, afya, biashara, n.k. Hata hivyo, protu hutumika visivyo pia kwa masuala kama vile wizi wa taarifa za siri, wizi wa nywila na udukuzi.[4] Mbinu za kubuni usanifu wa maombi ya mtandao hutumiwa. Programu ya wavuti ina sehemu za mteja na seva, na hivyo kutekeleza teknolojia ya "mteja-seva". Sehemu ya mteja inatekeleza kiolesura cha mtumiaji, huunda maombi kwa seva na kuchakata majibu kutoka kwayo. Marejeo
|
Portal di Ensiklopedia Dunia